BREAKING NEWS: Mbowe na Viongozi 5 CHADEMA Waachiwa Huru

BREAKING NEWS: Mbowe na Viongozi 5 CHADEMA Waachiwa Huru


Mbowe na wenzake ambao ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji na manaibu wake wa Bara na Zanzi­bar, John Mnyika na Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wote wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwemo mawili ya uchochezi wa uasi yanayom­kabili Mbowe na wanatarajiwa kuachiwa kwa dhamana leo. Mdee alikamatwa juzi Jumapili akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar wakati akiwasili kutokea nchini Afrika Kusini. Hata hivyo Mahakama imempa dhamana baada ya kuridhika na sifa za wadhamini. Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi ameomba kufanya marekebisho ya hati ya mashtaka ili kumjumuisha Mdee katika kesi inayowakabili viongozi wenzake sita wa Chadema wanaokabiriwa na mashataka manane yakiwemo ya uchochezi, uasi na kuhamasihsa maandamano, hivyo wote kwa pamoja watasomewa mashtaka upya. Masharti ya dhamana yalikuwa ni kila mshtakiwa kuwa wadhamini wawili watakaosaini bondi ya TZS 20m, barua ya utambulisho toka serikali za mtaa.

Aidha, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar ili kusomewa mashtaka yanayomkabiri. Viongozi wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe wametimiza masharti ya dhamana na kuachiwa huru katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Machi 3, 2018. Mahakama hiyo imejiridhisha na nyaraka za udhamini zilizowasilishwa mahakamani hapo. BREAKING NEWS: Mbowe na Viongozi 5 CHADEMA Waachiwa Huru

17 Replies to “BREAKING NEWS: Mbowe na Viongozi 5 CHADEMA Waachiwa Huru

  1. Viongozi chadema upeo wa fikra,mbinu zenu na usomi wenu na siasa zenu ndio mwisho kwenye maandamano tu ndio mmeona yatawakomboa ? Hamma mbadala wa namna nyingine? .kama kweli mnaona tz hatuko huru mmejitolea kuikomboa kwa nini nitumie mbinu za mwalimu baba wa taifa alivyotukomboa kwa ulaini bila maandamano wala vita?FIKIRINI UPYA,MTAFAKARI MTAPATA NJIA YA AMANI YA KUTUKOMBOA. NIKIWAANGALIA NAWAONA WASTARABU, MMESOMA,MNAJITAMBUA NA MNAMUABUDU MUNGU, MSIWE SABABU YA KUUMIZA WENGINE

  2. Mmefanyika dhahab safi. Nyie ni mashujaa ktk taifa letu.
    Kwangu mmepanda mbegu ya ujasir itakayoota na kuzaa matunda zaidi yenu, mimi nitaimwagilia maji na kuitunza hata itakapozaa zaidi.
    Makamanda peeeepo'z …????

  3. Naomba muwapitishie airport hawa waheshimiwa waone kile kitu walichotamani kisifike kimefika, ujuaji mwingi mwisho mtuingize kwenye machafuko. Na mkipewa nchi hamuwezi kutuongoza hata mwezi mmoja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *